Je dada unanifikiria?
Ama wajiona malkia
Nami binadamu asiyepewa hatia,
Ya kujitetea kimapenzi
Ila maneno sineni
Kesho unapata mchumba
Nami najifunga kwenye kijumba
Mlango wangu usifunguke tena,
‘Siombolee wala kutoa hela,
Ni matakwa ya mapenzi
Kushinda au kuenda,
Balaa ya bubu,
Ni mafanikio ya babu,
Aliyelipa mahari,
Johari yangu yatimia
Kesho yake pilau yapikwa
mbolezi yaimbwa
Mwanzo wa maisha yako
Mwisho wa maisha yangu
Staajabu hayo!
Msamiati
‘Siombolee - usiomboleze
mbolezi - nyimbo za mazishi
Malkia - queen
sifunguke - usifinguke
Siombolee - usiomboleze
hela - pesa
jahazi - ship
Disclaimer
The opinions expressed within the content are solely each author's and do not reflect the opinions and beliefs of the website or its affiliates.